Kipindi cha The Playlist cha
100.5 Times Fm kinaendelea na msimu wa Experience Africa kwa kuwashusha
wasanii wa Afrika mwezi huu ambao wanachagua nyimbo tano wanazozipenda
zaidi na kujibu maswali.
Baada ya kumsikia Orezi wa
Nigeria na R2bees wa Ghana Jumapili zilizopita, Jumapili hii kipindi
hicho kitamshusha gwiji wa muziki kutoka Afrika Kusini ‘Oskido’.
Oskido amejipatia umaarufu kwa
kazi zake za utayarishaji wa muziki, uandishi na uimbaji. Y-tjukutja ni
moja kati ya nyimbo maarufu hivi sasa zilizoandaliwa na Oskido.
“Niliwaahidi wasikilizaji kuwa
mwezi huu tutajikita katika kufanya mahojiano na kusikia nyimbo
wanazozipenda wasanii wakubwa wa Afrika waliopo nje ya Tanzania. Unajua
tumeshafanya na wasanii wa Tanzania ambao pia ni wakubwa kwa Afrika,
lakini tumeona tuupe umaalum mwezi huu wa nne tupate ladha ya wasanii
wengine wa nje ambao wanahit Afrika na hata huko duniani.” Amesema Omary
Tambwe aka Lil Ommy, mtangazaji wa The Playlist.
Kipindi cha The Playlist
kinakuwa hewani kupitia 100.5 Times Fm kila Jumapili kuanzia saa kumi
kamili hadi kumi na moja kamili jioni.
Fuatilia kwenye mtandao wa kijamii ( Instagram na Twitter) @LilOmmy @TimesfmTZ @OskidoIbelieve au sikiliza LIVE Online
www.timesfm.co.tz
About the Author
0 comments: